GET /api/v0.1/hansard/entries/942082/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 942082,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942082/?format=api",
    "text_counter": 354,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ruiru, JP",
    "speaker_title": "Mhe. Simon King’ara",
    "speaker": {
        "id": 13468,
        "legal_name": "Simon Nganga Kingara",
        "slug": "simon-nganga-kingara-2"
    },
    "content": " Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia mwanya huu nichangie jambo muhimu sana katika nchi yetu ya Kenya. La muhimu ambalo umefanya ni kutumia ujasiri na hekima yako kuleta maendeleo ya Kenya hasa kwa uwiano na uasiliano wa wakenya. Nchi nyingi duniani zimekua na misimamo yao mizito. Lakini katika Afrika, tumeshindwa kuwa na misimamo mizito. Kati ya misimamo hii ni lugha tunayotumia kuwasiliana sisi wenyewe. Kama vile waliongea mbele yangu walisema, wakati umefika wa Wafrika hasa Wakenya kujiamini na kuheshimu lugha za mawasiliano. Wakenya wengi ni wakulima. Lugha ambayo inatumika mashambani na viwandani ni lugha ya Kiswahili. Lakini hapa Bungeni, Kiswahili kinaonekana kuwa cha walio wadhoefu na Kizungu kinakaa kama cha wasomi. Mhe. Spika umesimama nasi na kukubali tuwe na maendeleo ya Kiswahili hasa katika Kanuni za Kudumu za Bunge kwa lugha ya Kiswahili. Hili ni jambo la kujivunia. Nimefurahi kwa sababu waliokua wanatumia lugha ya Kiswahili Bungeni walikua wachache sana. Umesimama nasi na ombi langu ni utenge muda maalum kila siku au kila wakati ambao Wabunge watakua wakitumia lugha ya Kiswahili ili Wabunge wote wakichukulie kama njia moja ya kuwasiliana katika Bunge na hata kule nje. Tukifanya hivyo, Kenya itatambulika. Kama tuvyojua, hata viongozi wetu, hasa kiongozi wa nchi, Uhuru Muigai The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}