GET /api/v0.1/hansard/entries/942087/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 942087,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942087/?format=api",
    "text_counter": 359,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Murang’a CWR, JP",
    "speaker_title": "Mhe. (Bi.) Sabina Chege",
    "speaker": {
        "id": 884,
        "legal_name": "Sabina Wanjiru Chege",
        "slug": "sabina-wanjiru-chege"
    },
    "content": " Mhe. Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii. Ni heshima kubwa. Bunge la 12 litakumbukwa na Wakenya kwa kuidhinisha Kiswahili. Najua wengi wetu tunaogopa kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu ya kuathiriwa na lugha ya mama. Ninaunga mkono Mheshimiwa kutoka Ruiru aliyesema kuwa itakuwa vizuri tukitenga siku moja ili tuzungumze kwa lugha ya Kiswahili ili tupate mazoea ya kuizungumza. Tunajua kwamba tunaruhusiwa kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili wakati wowote lakini tukijua siku kama ya leo tunafaa kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili, wengi wetu watajitahidi na tukienda pale nje, tutazungumza Kiswahili sanifu. Kwa sasa, ninasema hongera, Bw. Spika, na tuendelee kutukuza Kiswahili."
}