GET /api/v0.1/hansard/entries/942089/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942089,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942089/?format=api",
"text_counter": 361,
"type": "speech",
"speaker_name": "Shinyalu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Justus Kizito",
"speaker": {
"id": 71,
"legal_name": "Justus Kizito Mugali",
"slug": "justus-kizito"
},
"content": " Asante, Mhe. Spika. Kwa heshima na taadhima kuu, ningependa vilevile kuchangia Hoja hii na kuiunga mkono kwa sababu ni Hoja muhimu sana. Hoja hii itatupelekea sisi kuwa tunazungumza kwa lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha ya taifa na inatuletea ule uasili wetu kuona kwamba sisi kabisa ni Wakenya na tuna lugha ambayo inatuleta pamoja. Inatupatia ule mshikamano wa kitaifa ili tuweze kuenda mbele kama taifa linalozungumza lugha moja."
}