GET /api/v0.1/hansard/entries/942090/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 942090,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942090/?format=api",
    "text_counter": 362,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Shinyalu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Justus Kizito",
    "speaker": {
        "id": 71,
        "legal_name": "Justus Kizito Mugali",
        "slug": "justus-kizito"
    },
    "content": "Zaidi ya hapo, Hoja hii inaipatia lugha ya Kiswahili heshima yake na hadhi kubwa katika Kenya na hasa kuchochea wale wangependa kujifunza lugha hii. Kama mnavyojua, wanafunzi wengi hutumia lugha hii na mara nyingi huweza kuiga na kufuata mfano wa viongozi. Kama sisi viongozi tutakuwa tukitumia lugha hii katika Bunge hili, itakuwa nafuu sana na wanafunzi wale wanaweza kufuata mfano ule na kufanya tena utafiti zaidi na hata sisi kama Wabunge tutafanya utafiti mwingi zaidi ili tuweze kuzungumza lugha sanifu na kadhalika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}