GET /api/v0.1/hansard/entries/942091/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942091,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942091/?format=api",
"text_counter": 363,
"type": "speech",
"speaker_name": "Shinyalu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Justus Kizito",
"speaker": {
"id": 71,
"legal_name": "Justus Kizito Mugali",
"slug": "justus-kizito"
},
"content": "Jambo ambalo ningependa kusema ni kwamba lugha ya Kiswahili si lugha ya watu hafifu, si lugha ya wale akina pangu pakavu nitilie mchuzi, wale watu wa chini, hapana. Lugha ya Kiswahili ni lugha ya hata wasomi na kadhalika ijapokuwa hapa Kenya hatujakipatia Kiswahili nafasi kubwa hasa katika Bunge ili tuweze kukizungumza kwa wingi ili kuona kama ni cha mno. Kwa hivyo, ninashukuru sana Mhe. Spika. Unaingia moja kwa moja kwenye shajara ya historia na salua ya nchi hii kama Spika wa kwanza aliyetusaidia sana kuibua lugha ya Kiswahili na kuiweka katika ngazi ya juu. Kama unavyojua, kuna wengi wanajua Kiswahili hapa, wale tunawaita wakereketwa ama wakiritimba wa lugha ya Kiswahili. Ni wengi sana hapa lakini nafasi imekuwa kidogo. Ningependa kuhimiza na kuunga mkono Waheshimiwa wenzangu waliosema ni muhimu tutafute siku moja angalau tuweze kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili. La mwisho, ningependa tujue kwamba sisi tunasema kwamba tunataka kujilinganisha na Tanzania hasa katika usemi wa lugha ya Kiswahili. Ningependa kukuambia kwamba wale wakereketwa, wasomi wakuu katika lugha ya Kiswahili, wanapatikana Kenya. Kiswahili ambacho kimejaa ustandandi ni Kiswahili cha Wakenya. Kwa hivyo, tunapoangalia Kanuni hizi ama kaida hizi, lazima pia tuzipige msasa ili kuziainisha na lugha zetu na ile lahaja yetu ya Wakenya, sio ile ya Watanzania ambayo imeegemea sana upande wa Kiunguja. Sisi hapa Kenya kuna ule muegemeo wa upande wa Kimvita, kwamba Kiswahili chetu kina ustandadi mkubwa sana kushinda kile cha Tanzania."
}