GET /api/v0.1/hansard/entries/942093/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 942093,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942093/?format=api",
    "text_counter": 365,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii pia nichangia Hoja hii. Ninaungana na wenzangu kukupatia kongole kwa kuturuhusu kujadiliana Hoja katika Bunge hili letu. Ninataka kusema Kiswahili katika nchi yetu ya Kenya kilianzia mbali kwa sababu mahali penye nimezaliwa tulikuwa na makabila mengi sana na haikuwa rahisi kuwasiliana na wengine, ndiposa tukapata wasomi waliokuja hapo katikati wakatufanya tukifahamu Kiswahili na tukaanza kuongea na wengine. Wengi wamesema kwamba sio rahisi. Ni kweli Kiswahili sio rahisi. Lakini kwa wale wamejitolea kama wenzetu katika kamati hii kwa kutafsiri Hoja hii, wamefanya jambo nzuri sana. Katika michezo ya Afrika Mashariki, inawachukua Waganda muda mrefu sana kuwasiliana na Wakenya ama Watanzania kwa lugha ya Kiswahili. Itakuwa vyema sisi tukijifunza katika Bunge letu kuongea lugha ya Kiswahili kwa sababu wananchi wanatuelewa kwa manufaa ya Bunge letu. Mhe. Millie amesema kwamba tujifunze Kiswahili na tulete Sheng . Hatutaongea Sheng na Kiswahili. Tukifanya hivyo, tutakuwa tunachanganya wananchi kwa sababu kama tunaenda kujifunza Kiswahili katika Bunge letu, ni vizujri kiwe Kiswahili sanifu ili tuwasaidie wananfunzi. Tunaenda kwa kongamano nyingi na ni vizuri tuwe tunajua kuongea Kiswahili, kimombo au lugha ya ishara. Itatuwezesha kuwasiliana na watu vizuri. Ukikuja kule Trans Nzoia, kwa sababu ya makabila megi tunatumia Kiswahili. Nikimalizia, ninamshukuru Naibu wako kwa sababu anatupa ufahamu. Mheshimiwa Chris Wamalwa ameongea kuhusu matunda, lakini tunaidhinisha Kanuni hizi za kutusaidia katika Bunge letu ili tuweze kutafsri kwa lugha ya Kiswahili. Ninakushuru Mhe. Spika. Asante sana. Mimi pamoja na Wakenya wote na watu kutoka Trans Nzoia County tunakupa kongole. Ubarikiwe sana."
}