GET /api/v0.1/hansard/entries/942098/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 942098,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942098/?format=api",
    "text_counter": 370,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Mhe. (Bi.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Asante Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii ili niunge Hoja ya kuidhinisha Toleo la Kiswahili la Kanuni za Kudumu za Bunge la Taifa. Mwanzo, ninachukua nafasi hii nimwombee Mungu na nimpongeze Hayati Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta. Yeye ndiye aliyetoa amri Bunge la Kitaifa litumie Kiswahili. Kwa sababu hiyo, kama hangetoa amri, saa hii hatungekuwa tukiunda hizi Kanuni. Ni vyema tumtambue na tumwombee Mungu amweke pahali pema. Pili, ningependa kuzungumzia kidogo kwamba hili Bunge limekuwa likitumia Kiswahili kwa zaidi ya miaka 60. Ni kushukuru wewe kwa sababu baada ya hii miaka, sasa tuna hizi Kanuni za Kudumu. Pia, ningependa kupongeza lile jopo na Kamati ya Utaratibu na Masharti za Bunge ambayo pia mimi ni mojawapo. Mhe. Spika, ningependa kumrekebisha Naibu Spika aliyesema kwamba Kiswahili ni maskini. Kiswahili si maskini. Ni vile wanapenda kufanya mambo rahisi na kuomba kwa lugha jirani. Lakini Kiswahili kina lahaja tofauti tofauti kama vile Kipate, Kitikuu, Kisiu, Kiamu, Kimvita, Kijomvu, Kichichifundi ambacho chatoka Kwale na Kivumba ambacho kimetoka Vanga. Kwa hivyo, Kiswahili ni tajiri - ni vile tu wameziwacha hizi lahaja."
}