GET /api/v0.1/hansard/entries/942102/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942102,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942102/?format=api",
"text_counter": 374,
"type": "speech",
"speaker_name": "Muhoroni, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Onyango Oyoo",
"speaker": {
"id": 2408,
"legal_name": "James Onyango Oyoo",
"slug": "james-onyango-oyoo"
},
"content": "Wakicheka wanafikiria sielewi Kiswahili. Sehemu ninayowakilisha Bungeni inanibidi nijue Kiswahili kwa sababu kule ni uso wa Kenya. Kabila zote ziko hapo na mimi ndiye mkubwa wao. Sasa niko nao. Nakupongeza sana. Vile walisema ama kutaja hapo mbeleni, ningetaka iwe lazima tuwe na siku fulani ambayo tunachangia kwa Kiswahili kila wiki ili watu waongee kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu hii ni lugha ya taifa. Tena, tumepata nafasi ya kugundua wale walitumia njia ya mkato kufika Bungeni. Ni sharti mtu aelewe Kiswahili na Kizungu, lakini kuna watu hapa ambao hawakijui Kiswahili. Tunaanza kujiuliza jinsi walipata kuingia katika Bunge. Haya ni maneno ya Kiswahili. Walipita namna gani na hawaelewi Kiswahili vizuri? Chief Whip wangu haelewi Kiswahili vizuri."
}