GET /api/v0.1/hansard/entries/942107/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942107,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942107/?format=api",
"text_counter": 379,
"type": "speech",
"speaker_name": "Baringo CWR, KANU",
"speaker_title": "Mhe. (Bi.) Gladwel Chesire",
"speaker": {
"id": 13231,
"legal_name": "Gladwell Jesire Cheruiyot",
"slug": "gladwell-jesire-cheruiyot"
},
"content": " Asante sana Mhe. Spika. Pia, nimesimama kuwapa kongole wale wote wameunga Hoja hii mkono, ambayo, kupitia naibu wako, imetufanya tuzungumze kwa lugha ya Kiswahili. Naibu wako anataka Kanuni za Kudumu za Bunge zizinduliwe kwa lugha ya Kiswahili. Anaposema kwamba tunamshukuru Rais wa kwanza wa Kenya ambaye alitoa amri iwe haki ya wananchi kuongea kwa lugha ya Kiswahili Bungeni, ni vyema pia kukumbuka kwamba Rais wa pili wa nchi ya Kenya, Rais Daniel arap Moi, pia aliendeleza Kiswahili na akakifanya mashuhuri. Sikumbuki siku moja alipoongea lugha ya mama katika kazi yake. Alikuwa na huo moyo. Tunampongeza katika hiyo hali."
}