GET /api/v0.1/hansard/entries/942108/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942108,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942108/?format=api",
"text_counter": 380,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kuresoi North, JP",
"speaker_title": "Mhe. Moses Cheboi",
"speaker": {
"id": 329,
"legal_name": "Moses Kipkemboi Cheboi",
"slug": "moses-cheboi"
},
"content": " Nakushukuru sana, Mhe. Spika. Nikimalizia, nachukua nafasi hii kusema asante sana kwa waliochangia. Ni ajabu nimekuwa hapa kwa Bunge hili kwa miaka nyingi na sijapata kuona Hoja ambayo inaungwa mkono asilimia mia kwa mia. Hii ni mojawapo. Wabunge wote ambao wamezungumza hapo mbele wamechangia mambo tofauti, lakini wamesema kwamba inabidi tubadilishe kipengele ambacho kinasema umalizie Kiingereza ukianzia Kiingereza. Tunaweza kuchanganya lugha. Ni vizuri lakini pia tuchunge ili tusiweke mix kubwa mpaka tuwe na Sheng na kuileta katika Bunge letu. Hiyo itabidi twende kutafuta Kanuni tofauti za ile Sheng ."
}