GET /api/v0.1/hansard/entries/942166/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942166,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942166/?format=api",
"text_counter": 438,
"type": "speech",
"speaker_name": "Cherangany, JP",
"speaker_title": "Hon. Joshua Kutuny",
"speaker": {
"id": 61,
"legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
"slug": "joshua-kutuny"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika. Ni masikitiko sana kwamba tunaregesha tena kuzungumzia suala ambalo sheria ina mkondo wake. Mfumo na ufunuzi wa kutengeza bajeti upo. Kuna kuchukuliwa kwa maoni. Inakaliwa na kamati husika katika Bunge. Mswada unaletwa hapa, Makadirio ya Taifa yanajadiliwa, mwisho yanaidhinishwa. Kila kitengo kwa taifa kinapata kitita chake. Baada ya hiyo ni matumizi. Kwa Waziri kutoa nakala yake ni udhofu wa nidhamu. Ni kuzembea kwa kazi. Haki ya Mkenya kwa leo inapatikana kortini. Sisi sote tukiwa na tatizo lolote tunaenda kortini. Hatua ya kujaribu kupunguza fedha waliotengewa korti ni kuhujumu mahakama kutoa haki kwa Wakenya. Mhe. Spika, umesema kwamba tunapozungumza tutafute suluhu. Kuna Kamati husika ndani ya Bunge hili. Wamwite waziri wamuulize hatua yake inalingana na sheria ipi. Sisi viongozi ndani ya Serikali hatuwezi kukosana. Ni kama meno ya mbwa. Tuko marafiki kufa kuzikana lakini ikifika hatua zingine, tunaona kwamba wanahujumu utendakazi na upeanaji wa haki katika taifa la Kenya. Kwa hivyo, ningependa kamati husika kumwita Waziri na kumuuliza maswali. Hoja ambayo inaibuka ni kwamba kiranja wa mahakama ametoa ilani kwamba kutasitishwa kesi zingine ama mahakama haitajadili masuala fulani. Wana haki? Sisi kama Bunge, wakati kitita chetu kinaingiliwa na Serikali huwa tunafanya maandamano. Taifa lolote haliwezi kuruhusu kitengo cha usalama na kitengo cha korti kikome kwa sababu itahujumu haki ya taifa. Sheria ni lazima ifuatwe. Tuliidhinisha pesa hizi na hata sheria ya matumizi inayojulikana kwa lugha ya kimombo kama “Appropriations Bill” ilipitishwa na hakuna kitengo ambacho kina uwezo wa kukiuka na kupindua isipokuwa Bunge hili. Yeyote anajaribu kufanya yale anavunja sheria. Mimi ninaunga Serikali mkono. Hiyo inajulikana wazi na sihitaji kuipigia sifa, lakini inafika wakati lazima haki itendeke katika taifa la Kenya. Ndio sasa inanileta katika jambo lingine la kuzungumzia. Katiba tuliyonayo ambayo inalimbikiza mamlaka kwa kitengo kimoja cha taifa ni Katiba ambayo tunahitaji kama taifa ambalo linapiga hatua kuipiga msasa. Ninaweza kuzungumza kama mtu aliye na tajriba ya Bunge la Kumi ambapo mawaziri walikuwa ndani ya Bunge. Imefika wakati ambao ni lazima tuangalie Katiba tuliyo nayo - mawaziri watoke ndani ya Bunge kwa kuwa wao ndio wanajua matatizo ya wananchi. Kwa hivyo, tusikejeliane hapa. Tuzungumze na tuseme waziri aitwe na kamati husika na hatua ichukuliwe mara moja ili mahakama ipate kitita chake. Asante. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}