GET /api/v0.1/hansard/entries/942283/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 942283,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942283/?format=api",
    "text_counter": 111,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii nami nichangie Hoja hii. Mwanzo, ningependa kumshukuru Mhe. John Wambugu kwa kuleta Hoja hii muhimu nasi tuichangie. Tukitunga sheria ya kuwafanya asilimia 100 ya wanafunzi wanaotoka shule za upili kwenda vyuo, itakuwa jambo la muhimu sana na itakuwa msaada kwa Wakenya wote. Tunajua changamoto nyingi tunazozipata na vijana wanaharibikia hapo katikati. Kenya kuna nafasi nyingi za kazi ambazo vijana wanaweza kujishughulisha nazo. Nafasi na kazi ziko nyingi na husababisha Serikali kuchukua watu kutoka nchi zingine. Vijana wetu wakipelekwa katika vyuo hivyo kujifunza taaluma mbali mbali, ili wapate ajira na kuzongesha Kenya mbele. Vijana wako wengi katika nchi hii. Hata hivyo haitoshelezwi kamwe."
}