GET /api/v0.1/hansard/entries/942285/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 942285,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942285/?format=api",
    "text_counter": 113,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "wanajaribu kupeleka watoto katika National Industrial Training Authority (NITA) lakini kuna wengi wa kupelekwa ambao wako kule mashinani. Twajua hatari iliyoko kule Lamu. Vijana wengi wakimaliza shule za upili na wakose ile hamu au wavunjike moyo, wanaingilia matatizo mbali mbali ambayo yanajulikana. Inaleta utovu wa usalama katika nchi yetu ya Kenya tunayoipenda. Kwa mfano, inajulikana kwamba kule Lamu, vijana wengi wameingia katika mihadarati. Hatua hii ikichukuliwa, itapunguza pakubwa vijana kushiriki mihadarati kwa sababu hawana kazi ya kufanya. Tunapenda mambo kama haya lakini inakuwa ngumu kuyatekeleza kule Lamu. Wanafunzi walio katika shule za upili wanavuka kuenda kwenye vyuo vikuu. Lakini hata ile Hoja tuliyoipitisha ya watoto wa shule za msingi kwenda katika shule za upili bado hatujaweza kuitekeleza. Katika Lamu kuna Wadi ya Basuba ambapo mpaka sasa, kuna shule zimefungwa zaidi ya miaka mitano. Tungependa kwenda katika mpango huu mwingine. Nimeuliza swali ambalo ikifika wakati wa kujibiwa, linapelekwa katika kamati nyingine. Ni haki ya wale watoto kupata elimu. Sisi hatuombi. Ni haki yetu kwa watoto kule Lamu kusoma. Lamu ni Kenya. Wana haki kama watoto wa Kaunti zingine. Makala ya 53(1) (a) katika Katiba - ukiniruhusu nisome kwa Kiingereza, - inasema: “Every child has a right…"
}