GET /api/v0.1/hansard/entries/942298/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 942298,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942298/?format=api",
    "text_counter": 126,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Asante, Bwana Naibu wa Spika. Mheshimiwa Sankok, hivi karibuni utapata Standing Orders za Kiswahili ambazo zitakusaidia. Tulikuwa pamoja katika Kamati kwa hivyo utasaidika hivi karibuni. Itabidi usome Kiswahili zaidi na Kiswahili kitukuzwe. Nimeng’ang’ana na kuuliza maswali lakini hatujapata majibu mpaka leo. Hii itatusaidia sana. Hiyo asilimia ya wanafunzi wanaotoka shule za msingi na kujiunga na shule za upili bado haijatimia. Bado sisi kule Lamu tunavutwa nyuma. Naomba Serikali na wahusika waangalie Lamu kwa sababu sisi pia ni Wakenya. Sera nzuri zinawekwa lakini tutakuwa watu wa mwisho kufikiwa nazo. Kama vile Serikali inajitolea pakitokea shida katika shule hapa Nairobi, nao waje kule Lamu waone zile shida tunazopata; zaidi katika upande wa elimu. Ni haki ya wale wanafunzi kupata elimu. Ni jukumu la Serikali kuhakikisha kuna usalama. Naunga mkono Hoja hii. Itakuwa jambo la maana sana tukiifanya iwe sheria. Itatupatia ajira na vijana watapungua katika uhalifu."
}