GET /api/v0.1/hansard/entries/942783/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942783,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942783/?format=api",
"text_counter": 357,
"type": "speech",
"speaker_name": "Bura, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Wario",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mbeleni nilisimama kwa Kifungo 43 cha Kanuni ya Bunge kuomba fursa ili nizungumzie tatizo linalokumba watu wangu. Mnamo tarehe 22 na 23 za mwezi huu, National Police Service pamoja na Serikali Gatuzi ya Kitui, asubuhi na mapema, walivamia vijiji vitatu ikiwemo Inyali, Kiwanja na Kalalani. Walibomoa miji na nyumba zaidi ya elfu moja. Naibu Spika wa Muda, ninapozumgumza sasa hivi, kuna watu zaidi ya elfu tano ambao nyumba zao zimebomolewa. Hawana maji, chakula wala mahali pa kulala. Wanakaa chini ya miti. Shule za Umma tatu zikiwemo shule ya Inyali, Did-Ade na Kalalani zimebomolewa. Naibu Spika wa Muda, iwapo wafugaji na wananchi hao wamefanya hatia, ni mahakama gani imetoa amri ya kubomolewa kwa nyumba zao? Ni mahakama gani imetoa amri ya kubomoa shule ambazo watoto wa Taifa letu la Kenya wanasomea? Ninavyozumgumza sasa hivi, Wakenya wanang’ang’ana na watoto wao wafanye mtihani. Lakini kwingine, watoto wa Inyali, Kiwanja na Kalalani hawana mahali wanaita shule. Hii ni kwa sababu Inspekta Mkuu wa Polisi akishirikiana na Gavana wa Kitui wamebomoa shule zao. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, msafara wao hauishii hapo. Wao wanaelekea miji inaitwa Kaniki, Gurujo na Basahargesa katika eneo langu la Bunge. Tulipouliza ni kwa nini shule zilibomolewe tulielezwa maneno mawili: Kwanza, niliambiwa kuwepo kwa wafugaji katika sehemu hiyo ni tishio kwa usalama wa jamii jirani."
}