GET /api/v0.1/hansard/entries/942799/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942799,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942799/?format=api",
"text_counter": 373,
"type": "speech",
"speaker_name": "Garsen, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Guyo",
"speaker": {
"id": 13336,
"legal_name": "Ali Wario Guyo",
"slug": "ali-wario-guyo-2"
},
"content": ", Tana Primate Reserve na Kipini Conservancy . Tuko na game reserves na conservancies zaidi ya nusu ya Tana River. Sisi tunaishi vizuri na majirani wetu. Hata ndiyo maana mara nyinyi Tana River humpigia Kalonzo Musyoka kura kwa sababu ni jirani wetu. Sasa Mhe. Nyamai, IG Mutyambai ambaye ametoka hiyo sehemu pamoja na Governor Charity wamechukua nafasi hii kuwadhulumu watu wa Tana River. Mama anafaa kuwa na huruma lakini huyu ameonyesha wazi hana huruma. Saa hii wamama wenzake na watoto wao wako kwa baridi. Lakini yeye anaongea hapa kama wale ndio wauaji. Je, watu wa Kalalani ama Inyali ni wauaji? Watu wa Tana River ni wakarimu sana. Lakini huu ukarimu wetu usichukuliwe kuwa uoga. Sisi tunasema kwamba Serikali ichukue hatua na Mutyambai ajiiuzulu kwa sababu hafai kuwa Inspector-General wa Polisi. Ametakesides. Kwa vile Mhe. Nyamai na Mhe. Charity wanatoka kwa jamii yake, wameshirikiana kukandamiza watu wa Tana River. Kwa hivyo, Mutyambai kwanza ajiuzulu na Serikali ichukue hatua dhidi yake. Asante sana."
}