GET /api/v0.1/hansard/entries/942892/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942892,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942892/?format=api",
"text_counter": 42,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Statement hii ambayo imeletwa hapa na Sen. Faki wa Mombasa County. Kusema ukweli, bodi hii ambayo imechaguliwa na Waziri, ukiangalia vizuri sana, sio sawa kwa sababu watu wa Mombasa hawakujumulishwa au kuhusishwa. Hata Seneta wa Mombasa mwenyewe ambaye ndiye mwenye kaunti hakujulishwa wala watu wa Mombasa hawakujulishwa kwamba kuna kwamba Waziri anataka kubuni bodi ya usimamizi. Mimi kama Seneta wa Kwale pia namuunga mkono Seneta wa Mombasa kuhusu taarifa hii ambayo ameleta kwa Bunge hili la Seneti. Kwa hivyo, pale ambapo utakapoelekeza kwamba hiyo Kamati ichunguze habari hii bodi, basi, ichunguzwe vizuri waangalie hao waliowekwa hapo ni nani. Hii ni kwa sababu watu wa Mombasa wana haki yao na watu wa nje wana haki yao. Wanafaa kujua ni nani ambao wamewekwa katika hiyo Bodi."
}