GET /api/v0.1/hansard/entries/943093/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 943093,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/943093/?format=api",
"text_counter": 243,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bw. Spika, kuna swali ambalo najiuliza. Seneti imetoa uamuzi wake. Je, tunaelewa mgogoro ulioko kule Taita Taveta? Uamuzi wetu ni kuwa madai yaliyoletwa hayana msingi wowote. Ukweli ni kwamba kuna mgogoro katika Kaunti ya Taita Taveta. Licha ya kuwa tumesema kuwa madai yaliyotolewa hayana msingi wowote, tunafaa kuwaunganisha watu wa kaunti hii. . Mimi ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ugatuzi na Mahusiano ya Kiserikali. Tulijaribu kuwaunganisha. Tulifanya hivyo mara si moja. Tulikutana na Wawakilishi wa Wadi na Naibu wa Gavana ili kujaribu kuwaunganisha. Hata hivyo, Seneti imeeleza katika Ripoti yake kwamba madai yaliyotajwa hayana msingi wowote. Hiyo itampa gavana nguvu nyingi. Huenda ataonyesha kuwa Wawakilishi wa Wadi hawawezi kufanya chochote. Sisi kama Seneti tumekubaliana mia kwa mia. Ripoti inasema kwamba wakati gavana alipokuwa akisoma hotuba yake, alisema kuwa kisheria anaweza kuvunja Bunge la Kaunti ya Taita Taveta. Wanakamati wameeleza kuwa aliwahadaa wananchi wa Taita-Taveta. Licha ya kuwa nitajumuika katika kuwaunganisha, pengine tungeeleza katika hii Ripoti kuwa tulipata maoni yao. Inafaa kuwekwa wazi kuwa gavana aliitwa lakini hakuja. Tunafaa kuwaunganisha watu wa Taita Taveta ili shughuli ziendelee. Kuna Seneta ambaye alisema kuwa walikuwa wakiongea lakini kukawa na mtafaruku kuhusiana na kuondolewa kwa gavana mamlakani. Tumetoa maoni yetu lakini Wawakilishi wa Wadi wanafaa kwenda kortini. Tumefanya kazi yetu kama Seneti lakini pengine tungependekeza kuwe na umoja ili Kaunti ya Taita Taveta iweze kuendelea mbele kwa sababu kisheria kazi yetu ni kutetea ugatuzi. Hilo ndilo jambo ambalo tunafaa kufanya. Hata hivyo, naunga mkono Ripoti hii ambayo tumepitisha kwa asilimia. Nawapongeza Wanakamati kwa kazi waliofanya. Ijulikane wazi kwamba kitakuwa kizungumkutu kujaribu kuwaunganisha watu wa Taita Taveta. Huenda gavana akasema kwamba hana makosa na yeye ni mweupe kama pamba kwa sababu Seneti iliamua. Ikiwa hivyo, itakuwa vigumu sisi kujaribu kuwaunganisha. Huenda gavana atawaambia kuwa Seneti ilisema kwamba hana makosa na kwamba walio na makosa ni wale walioleta ripoti katika Seneti. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}