GET /api/v0.1/hansard/entries/943265/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 943265,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/943265/?format=api",
    "text_counter": 18,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "kwamba ardhi yao imekua kama mbuga ya wanyama. Kila mtu ni mgawo; kila mtu ni kinyang’anyiro. Hivi sasa, watu wa Lamu hawana mahali popote pa kuishi. Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba, vipande vikubwa sana vya ile ardhi ya Lamu vimechukuliwa na mabepari. Na hao ambao sio wengine, lakini ni Waafrika weusi, na ni Wakenya matajiri ndani ya Serikali ya Kenya. Pia, kumekuwa na ugawanyaji wa mashamba. Hivi sasa, tunaona kwamba baada ya kuporwa yale mashamba, sasa kumeingia jambo la kutengenezwa kwa bandari ya Lamu. Bw. Spika, ni jambo la kusikitisha pia kwamba, sisi kama watu wa eneo la pwani, tumetegemea sana uvuvi. Uvuvi, kama ulivyotajwa ndani ya Kauli ya Sen. Loitiptip, ni jambo linalonishika mimi kwenye roho. Hii ni kwa sababu watu kama sisi tumesomeshwa na mambo ya uvuvi. Kwa hivyo, ni jambo la kusikitisha kuona kwamba hivi sasa mashimo yametobolewa ndani ya ile bandari, na samaki wote wametoroka. Kwa hivyo, wavuvi hawana kazi ya kufanya, watoto wamebaki ndani ya majumba, bibi zetu wengine na mama zetu washakwenda kwa sababu mvuvi hawezi kupata haki yake. Bw. Spika, naiunga hii Kauli ya Sen. Loitiptip mkono, ya kwamba, yale malipo ya ridhaa kwa sababu ya kuharibiwa kwa biashara na ardhi yake, ni jambo ambalo Serikali lazima izingatie. Kumekua na upungufu Zaidi. Mara nyingi Serikali husema: ‘Kesho, kesho kutwa.” Lakini hata ukiangalia zaidi, utaona kwamba hata yule mkubwa wa hiyo bandari ---. Ijapokuwa vijana wetu wa Lamu wanajua mambo hayo ya kuogelea, mambo ya bandari na kila kitu; hata wako na degree katika usimamizi wa bandari, lakini hao pia hawako katika ile msururu ya kwamba wanaweza kujiongozea ile bandari iliyoko kwao. Sheria na Katiba yetu inasema kwamba, ikiwa kutakuwa na mtu katika lile eneo, basi apewe nafasi hiyo. Hii ni kwa sababu kilio chake ndio sawa sawa na kile kilio cha Mu-Amu. Kumalizia, Bw. Spika, ni kwamba, yale maeneo yaliyotengwa hivi sasa ili kutengezwa hii bandari, na ambayo yameharibu biashara, wale wavuvi lazima wahesabiwe. Hesabu hii lazima iwekwe kinaga ubaga ili tujue ni wangapi – na hao wenyewe wanajuana kule nyumbani – ili waweze kufikiriwa ili wapate hayo mapato yao kwa sababu ya kuharibiwa hizi biashara. Asante."
}