GET /api/v0.1/hansard/entries/943266/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 943266,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/943266/?format=api",
    "text_counter": 19,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Kauli hii iliyoletwa na Seneta mwenzetu wa Lamu, Sen. Loitiptip. Kusema ukweli, hili ni jambo la kusikitisha sana, kwa sababu, mpaka sasa, kuna watu wengine wa Lamu ambao hawajalipwa ridhaa yao. Miradi imefanywa, na ukiangalia kabisa, shida iko katika National Land Commission (NLC), kwa sababu hakuna uwazi wala ukweli. Kwa hivyo, naiunga mkono Kauli iliyoletwa hapa na Mhe. Loitiptip, kwa sababu mimi, kama Seneta wa Kwale, nina shida kama hiyo. Hivi sasa huko Kwale, kuna lile Bwawa la Mwache na pia kuna hiyo barabara itakayojengwa ya Dongo Kundu, na wananchi wengi pia bado hawajalipwa hadi sasa, ingawaje kuna baadhi yao ambao wamelipwa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}