GET /api/v0.1/hansard/entries/943696/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 943696,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/943696/?format=api",
    "text_counter": 449,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Nikirudi kwa Arifa iliyoletwa na Seneta wa Makueni, ningependa kuiunga mkono kwa jambo moja. Kwanza, ningependa kukemea uamuzi wa Serikali wa kuvunja Bodi ya usimamizi ya Kenya Ferry Services. Wameondoa wale waakilishi ambao ni raia, ambao ni members of the public, yaani wananchi wa kawaida, lakini wakaacha wale watumishi wa Serikali ambao wanakaa katika Bodi ile. Kwa mfano, kuna Katibu Mkuu ama Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Fedha ambaye anakaa katika Bodi ya Kenya Ferry Services. Kuna Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Usafiri na Uchukuzi ambaye pia anakaa katika Bodi ile na kuna mwakilishi kutoka Shirika la Kenya Ports Authority; wote wanakaa katika Bodi ile. Kwa hivyo, wakati wengine walipokuwa wanapelekwa nyumbani, hawa pia walikuwa wanafaa kwenda nyumbani kwa sababu wao wamehusika pakubwa katika maamuzi yote ambayo yamefanyika katika Bodi ya Kenya Ferry Services. Jambo la pili ni kwamba mpaka sasa Shirika la Kenya F erry ama Wizara ya Uchukuzi haijatoa chanzo ama sababu ya ajali ambayo ilitokea. Itakumbukwa kwamba mnamo mwaka 1994, kulikuwa na mkasa wa ferry kama huu na wakati ule, Serikali iliunda Tume ambayo iliongozwa na Jaji Mbogholi kuchunguza swala lile. Tume ile ilifanya uchunguzi wake na ikatoa mapendekezo yake kwa Serikali lakini mpaka leo, mapendekezo hayo hayajatekelezwa. Bi. Spika wa Muda, kwa sasa hatuwezi kuwalaumu wasimamizi wa Kenya Ferry Services kwa sababu kuchunguza swala kama lile, unahitaji utaalamu tofauti tofauti ambao kwa sasa hakuna katika Shirika la Kenya Ferry Services."
}