GET /api/v0.1/hansard/entries/943702/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 943702,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/943702/?format=api",
    "text_counter": 455,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Mombasa. Hii ni kama kuweka pikipiki katika Thika Super Highway ambapo unaona pikipiki zinaruka wakati magari makubwa yanapita na kurudi. Kwa hivyo, katika kivuko cha feri, mpaka sasa kuna hatari kubwa ya wananchi kupata hasara kwa sababu pale katika kivuko, meli kubwa ambazo zinaingia kuleta mizigo katika Bandari ya Mombasa zinatumia sehemu ile na hakuna njia yoyote ambayo mpaka sasa Serikali imefanya kudhibiti ajali ambazo zinatokea katika sehemu ile. Bw. Naibu Spika, nilitangulia kusema wakati nilipotoa taarifa tarehe moja mwezi huu kwamba uwekezaji wa Serikali katika Shirika la Feri umekuwa duni sana. Katika bajeti ya Kshs1.2 billion, Serikali inatoa Kshs400 million pekee, ambapo pesa zile zinatakikana zitolewe kuhakikisha kwamba feri zimeekwa katika hali ambayo ni salama kwa wale wanazozitumia kila siku. Kila siku, feri inavusha raia 300,000 kutoka Likoni na kurudi. Kwa hivyo, feri ni kivuko muhimu ambacho kinasaidia usafiri kati ya Mombasa na nchi jirani ya Tanzania. Ni kiungo muhimu ambacho kinasaidia usafiri kwa watalii wanaoenda kujivinjari maeneo ya Diani na pia ni kiungo muhimu ambacho kinasaidia kuunganisha Kaunti ya Mombasa na Kaunti ya Kwale. Asante Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii."
}