GET /api/v0.1/hansard/entries/943706/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 943706,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/943706/?format=api",
    "text_counter": 459,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii niweze kuchangia pia. Kitendo au mkasa uliotokea haukuwa mkasa mzuri katika nchi yetu. Kusema ukweli, mkasa ulitokea kwa bahati mbaya lakini kwa vile kitendo kama kile kimetokea, lazima tuzungumze kama viongozi. Wakati hii ajali ilipotokea nilikuwa safarini nje ya nchi kule Estonia. Niliona habari hii kwa mtandao lakini niliporudi, siku ya pili nilienda mpaka pale kwa afisi ya Kenya Ferry Services na tukafanya mkutano na Board of directors na mkurugenzi wa Kenya Ferry Services . Kusema ukweli, tusiwalaumu wakurugenzi wa Kenya Ferry Services; wamefanya kazi yao kiusawa kabisa; haswa Mkurugenzi wa Kenya Ferry, Bw. Bakari. Siku hiyo nilikuwa na Mkurugenzi, Bw. Bakari na Chairman; Bw. Danson Mwazo. Niliongea nao na nikawapongeza kwa kazi waliofanya. Wamekuwa pale kutoka wakati kile kisanga kilitokea mpaka wakati maiti zilipatikana. Mimi kama kiongozi ambapo pia hicho ndicho kivuko changu kwenda kwenye Kaunti yangu ya Kwale, nikitoka Nairobi, ni lazima nivuke ferry kuenda Kwale, hakuna njia nyingine. Kwa hivyo, Serikali inapaswa kuteuwa tume maalum ichunguze The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}