GET /api/v0.1/hansard/entries/943707/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 943707,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/943707/?format=api",
    "text_counter": 460,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "kinaganaga mkasa huu ulitokea namna gani. Hii tume inafaa kutoa habari kwa Serikali na nchi yetu tukufu. Bw. Naibu Spika, ningeomba Serikali iteuwe tume ichunguze hii ajali ilitokea namna gani kuliko kulaumiana, kulaumu bodi, au wakurugenzi wa Kenya Ferry Services ambao ni wanadamu kama sisi. Wamefanya hii kazi kwa uzuri sana. Mimi mwenyewe nilikuwa pale, nikamuona Mkurugenzi wa Kenya Ferry, Bw. Bakari, na Mwenyekiti; Bw. Mwazo, aliyekuwa Seneta wa Taita Taveta zamani. Nilizungumza nao na wamefanya hiyo kazi kwa kweli kabisa. Pia, ningependa kuwapongeza wanamaji wetu wa Pwani waliofanya kazi nzuri sana. Kwa hivyo, tusilaumiane hapa. Tuunde kamati au tume ya kuchunguza mkasa hu una kutoa ripoti kamili kwa Serikali. Asante, Bw. Naibu Spika."
}