GET /api/v0.1/hansard/entries/943826/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 943826,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/943826/?format=api",
"text_counter": 35,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii ili kuchangia Hoja ya Sen. Nyamunga kuhusiana na wafanyikazi wanaohudumia jamii kwa mambo ya kiafya. Bw. Spika, wengi wetu waliozaliwa katika miaka ya sitini walipitia mikononi mwa wakunga, ambao ndio waliokua wafanyakazi wa kwanza wa jamii waliokuwa wakisaidia katika masuala ya afya. Hadi sasa, wakunga hawa bado wako katika jamii ambazo ziko mbali na mahospitali. Wakunga hawa wanasaidia pakubwa kuzalisha bibi, dada na mama zetu, ili wapate watoto. Njia wanayotumia sio salama, lakini ndio njia pekee wanayoweza kusaidia ili kuhakikisha kwamba wameweza kupata watoto. Bw. Spika, baada ya janga la UKIMWI kutuingilia, wafanyikazi wa afya wa kijamii waliongezeka. Wanafanya kazi hizi katika kila mji, wengine bila malipo, na wengine katika hali ambayo inatoa athari kubwa kwa maisha yao. Hii ni kwa sababu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}