GET /api/v0.1/hansard/entries/943827/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 943827,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/943827/?format=api",
"text_counter": 36,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "hawana vifaa vya kujikinga na magonjwa ambayo wanayohudumia kwa Wakenya wengine. Bw. Spika, Hoja hii imekuja wakati mwafaka kwa sababu tumeona kwamba katika kaunti nyingi, wafanyakazi wa afya wa jamii hawana malipo. Serikali za kaunti hazijakuwa na rasilimali za kutosha za kuhakisha kwamba wameajiri kazi wafanyakazi ambao watahudumia wananchi katika kila zahanati ama hospitali. Katika kaunti nyingi, wengi wa ngariba ambao wanapasha vijana tohara ni wafanyakazi wa afya wa jamii lakini hawashughulikiwi kwa njia yoyote na serikali hizo. Bw. Spika, tumeona kwamba ziko baadhi ya kaunti ambazo zimeweza kuwajali wafanyakazi kama hawa. Wanawakatia kadi za NHIF ili wakiwa na matatizo ya kiafya, wanaweza kwenda kuhudumiwa katika hospitali za Serikali bila ya malipo yoyote. Jambo hilo halitoshi kwa sababau pia wanahitaji kula, kuvaa, na watoto wao wanahitaji kwenda shule. Iwapo hawatalipwa kiinua mgongo kwa kufanya kazi hii, basi itakuwa ni kazi bure kwa sababu watavunjika mioyo. Baada ya muda fulani, hakutakua na watu waliojitolea kama hao. Bw. Spika, tulipokuwa na mkurupoko wa ugonjwa wa chikungunya kule Mombasa, wafanyakazi wa kiafya wa jamii walitumika pakubwa. Walihakikisha kwamba maeneo wanamoishi binandamu yamepigwa dawa, kumekuwa salama na ugonjwa huo ukaondoka Mombasa kabisa. Bw. Spika, naunga mkono Hoja ya Sen. Nyamunga, na naomba kwamba asiachie hapo. Hata kama ni sheria kupitishwa ili tuhakikishe kwamba wafanyakazi wa afya wa jamii wanapata ruzuku kila mwezi, itakua ni jambo kubwa sana la kuwasaidia wanaojitolea kwa kazi zao kwa sasa. Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Naunga mkono."
}