GET /api/v0.1/hansard/entries/945446/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 945446,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/945446/?format=api",
    "text_counter": 205,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Hoja ya kumpongeza Eliud Kipchoge, Brigid Kosgei pamoja na wanariadha wengine ambao waliipa Kenya sifa kubwa kule Doha. Bw. Naibu Spika, kabla ya kutoa mchango wangu, mnamo siku ya Ijumaa jioni, wanajeshi wetu wa Jeshi la Wanamaji waliweza kufaulu kupata miili miwili ya Mariam Kighenda na bintiye Amanda ambao walikuwa wamezama mnamo tarehe 29 Oktoba, 2019. Lilikuwa ni jambo ambalo liliwatamausha sana Wakenya wengi. Hata hapa Bungeni tulipolizungumzia, wengi wetu walitamaushwa na hali ilivyokuwa inaendelea. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}