GET /api/v0.1/hansard/entries/945449/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 945449,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/945449/?format=api",
    "text_counter": 208,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Kama nchi tuliweza sote kuacha kazi zetu na tukakaa kuangalia Mkenya huyu ambaye alikuwa Vienna akiipa nchi hii umaarufu mkubwa kwa kazi aliyoifanya kwa juhudi zake peke yake. Tumeona kwamba Wakenya wengi ambao wanashiriki katika mbio tofautitofauti ulimwenguni, iwe ni Chicago, Berlin au mahali popote, huwa na uzalendo mkubwa. Wakati wanapeperusha na kujifunikia bendera ya nchi ya Kenya, sisi huona fahari ya nchi yetu. Lakini jambo hilo linaishia pale pale. Hata Wizara yetu ya Utalii haijaweza kuchukua rasilimali kama hii kuhakikisha kwamba Kenya inapata umaarufu na watalii wengi wanakuja kuangalia vitu vingi vya kitalii hapa nchini."
}