GET /api/v0.1/hansard/entries/945828/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 945828,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/945828/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Samburu CWR, KANU",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Maison Leshoomo",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "ya wanyama. Ni muhimu kwa sababu wafugaji wa wanyama wanaumia kwa sababu hawana njia yoyote ya kufaidika au kusaidia familia zao kutokana na wanyama wao. Wale wanaokuza miwa, majani na kahawa wako na njia zote za kujisaidia. Wana soko. Kwa mfano, kuna soko la Kahawa ya Kenya katika kila nchi. Tukipata bodi inayoweza kuwasaidia wafugaji wa wanyama, watapata njia za kufaidika. Tunajua vizuri sana kwamba wafugaji wa wanyama humu nchini hawana njia yoyote ya kujifaidisha isipokuwa kutokana na hao wanyama. Kule Samburu ninakotoka na katika sehemu nyingine kama Laikipia, Turkana na Pokot, utaona wanyama wanapigwa risasi kama wanyamapori. Kwa sababu hakuna nyasi, huwa wanauliwa kama wanyama wa mwituni. Hata wanyamapori hawauliwi jinsi wanyama wetu wanavyouliwa wakati wa ukame. Tukipata bodi inaweza kutusaidia kujua ni njia gani mfugaji anaweza kujisaidia nayo kutokana na wanyama anaofuga. Wafugaji hawana shamba lingine. Shamba lao ni hao wanyama wao. Kunapaswa kuwa na vichinjio katika kaunti zao ili wapate mahali pa kusafirisha nyama. Hata wakiwa na maziwa, hawana mahali pa kuyasafirisha. Itakuwa muhimu sana tukiwa na bodi hiyo kwa sababu itatusaidia na kuwasaidia wafugaji. Inafaa Serikali ianze kutafuta soko la kusaidia wafugaji wapate mahali pa kuuzia wanyama wao. Masoko yanapatikana kila mahali mnyama yuko lakini wanajinunulia wenyewe tu. Hakuna mahali pa kuuza wanyama wao na wapate pesa nzuri. Kenya Meat Commission ilikufa kitambo. Haina mahali popote. Hata wanyama wakipelekwa huko, watu wanaweza kukaa hata miezi sita au mwaka mmoja bila kulipwa. Zile kilo za nyama wanapeleka KMC ni za kuumiza. Kuna wafugaji wengine Wazungu kule Laikipia. Wakipeleka ng’ombe wao, huwa wanatoa kilo 500 au 600 na wetu wanatoa kilo 200. Hatuna njia ya kuwafunza wafugaji wetu jinsi ya kuwalisha ng’ombe wao ili wapate kilo hizo. Kwa hivyo, wafugaji wanaumia. Vita tunavyopigana kuhusu wanyama wanaoibiwa ni kwa sababu ya umaskini. Una mali – ng’ombe na mbuzi – lakini huna mahali pa kuwauza. Huna mahali unaweza kujisaidia. Ingekuwa vizuri tupate bodi hiyo ili izingatie mambo ya wanyama kwa sababu ni muhimu sana wafugaji wafaidike. Naunga mkono Mswada huu."
}