GET /api/v0.1/hansard/entries/946651/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 946651,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/946651/?format=api",
    "text_counter": 337,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "na vile walifanya hadi mwisho. La haula, wakisema kwamba wanaanzia maswala ambayo yamewekwa katika mjadala peke yake bila kuangalia huko nyuma, basi kuna wananchi ambao tunawaakilisha ambao hawatakuwa wamesikizwa. Ndio maana nafikiri rafiki yangu, Sen. Cheruiyot, amesema kwamba ninatetea upande fulani. Mimi sitetei upande wowote, lakini kuna wananchi waliomchagua yule gavana. Ni wale wale wananchi waliowachagua wale Members of County Assembly ( MCAs ). Je, gavana na wale wananchi walisikizwa? Kuna hali ya kuleta maoni yao katika sheria, ili kujua kwamba wananchi wenyewe wako na gavana au upande wa MCAs. Jambo hili halikufanyika. Kwa hivyo, ninatumai kwamba wakati Kamati hii itaanza kazi, watu hao wote watapewa nafasi ili walete maoni yao. Hilo ndilo lilikua shauku yangu. Asante, Bw. Naibu Spika."
}