GET /api/v0.1/hansard/entries/947275/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 947275,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/947275/?format=api",
"text_counter": 56,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii ili nichangie katika malalamiko yalioletwa na Mkenya ambaye ni mzalendo kamili. Malipo ya NYS ni donda sugu katika uchumi wetu kwa kuwa watu wengi waliopata kazi hizi bado hawajalipwa. Jambo hilo pia linaathiri pakubwa kaunti zote nchini kwa sababu wengi wa wale ambao hawafanyi miradi ghushi wanachelewa kulipwa, ilhali wanaofanya miradi ghushi wanalipwa mapema. Bw. Spika, ukiangalia gazeti la Daily Nation kila Jumatatu na Jumanne, utapata matangazo mengi – karibu kurasa kumi – ya kunadiwa kwa mali ya watu ambao wamechukua mikopo ya kufanya biashara na serikali za kaunti pamoja na Serikali Kuu. Kwa hivyo, ipo haja ya kupambana na swala hili kwa dharura, kwa sababu--- The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}