GET /api/v0.1/hansard/entries/947558/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 947558,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/947558/?format=api",
    "text_counter": 339,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Haji",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 26,
        "legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
        "slug": "yusuf-haji"
    },
    "content": "Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja hii ambayo imependekezwa na Seneta Kasanga kuhusu kuanzishwa kwa vyama vya jamii vya kulinda misitu katika kila kaunti. Kwanza, nampongeza Seneta Kasanga kwa kuleta Hoja hii katika Bunge kwa sababu imekuja kwa wakati mwafaka, wakati tunaona kwamba kuna misukosuko kila mahali kuhusu misitu. Kuna misukosuko katika sehemu za Mau na sehemu zingine ambazo kuna hatari kubwa kwa misitu yetu kupotea. Bi. Spika wa Muda, kule Mombasa, tuna misitu ya mikoko, yaani, Mangroove"
}