GET /api/v0.1/hansard/entries/947567/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 947567,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/947567/?format=api",
"text_counter": 348,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Haji",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 26,
"legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
"slug": "yusuf-haji"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Nilikuwa nasema kwamba kule Mombasa tuna misitu ya mikoko ambayo inasaidia pakubwa kwa kusafisha hewa na vile vile kusaidia sehemu ambazo samaki wanataga mayai ili waweze kuzaana na kuendela kutoa chakula na kuweka sawa yale mazingira ya baharini. Bi. Spika wa Muda, ukiangalia sehemu kubwa katika eneo la Tudor, kuna sehemu kubwa ya msitu wa mikoko ambao umekatwa ili wananchi waweze kupata makao. Hii inaathiri pakubwa sehemu za samaki kuzaa na kutaga mayai na hivyo, inapunguza idadi ya samaki ambao wako katika Bahari ya Hindi ambao wanatumia mikoko ile ili waweze kuzaaa na kutaga mayai. Kumekuwa na mvutano baina ya wale wakaazi halisi wa sehemu zile ambao wengi ni wavuvi na wengi wanafanya ukulima wa nyuki ili waweze kupata asali ya mikoko. Katika sehemu zile za mikoko ambazo zina misitu, kuna nyuki wengi ambao wanasaidia kupatikana kwa asali katika mji wa Mombasa. Lakini utapata kwamba ile mikoko inapokatwa, sehemu zile ambazo watu wangeweza kuweka mizinga yao na kupata nyuki wa kuweza kuzalisha asali na vile vile samaki zinaendelea kupungua. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}