GET /api/v0.1/hansard/entries/947568/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 947568,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/947568/?format=api",
    "text_counter": 349,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Haji",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 26,
        "legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
        "slug": "yusuf-haji"
    },
    "content": "Hoja hii itasaidia pakubwa kuwapa watu asili wa sehemu zile - kama alivyotangulia kusema Sen. Cheruiyot - nafasi ya kusimamia ile misitu kwa sababu wanajua vile watatunza misitu ile na kusaidia pakubwa kuleta ajira katika sehemu zile. Ukiangalia katika sehemu ya Mombasa hivi sasa, kuna sehemu kubwa ambapo kuna takataka ambayo ni hatari kwa mazingira kwa mfano zile plastic ambazo zinatupwa katika bahari ili wale waweze kuweka misingi ya nyumba zao. Jambo hili linaharibu mazingira ya bahari. Mara nyingi, bahari inatoa fursa ya kuondoa uchafu wote wakati zile mawimbi zinakuja katika ufuo ili kuondoa takataka na pia kusafisha mazingira. Lakini utapata kwamba takataka nyingi ambazo zinatupwa katika bahari zinasaidia wale ambao wanaweka makao katika sehemu zile ili waweze kujenga nyumba zao. Hii ni kwa sababu huwezi kujenga nyumba kwenye maji. Wanatupa takataka ambazo zinakaa kama msingi na baadaye wanaanza kujenga nyumba zao. Kwa hivyo, Bi. Spika wa Muda, hii itasaidia pakubwa kuwapa nafasi wale ambao wanachunga misitu kama hii ya mikoko kuhakikisha kwamba mazingira au misitu ile haiharibiwi. Pia, tumeona kwamba kumekuwa na utepetevu ama ulegevu kwa upande wa Kenya Forest Service kwa kuzuia watu kukata misitu na vile vile kulinda misitu ile ambayo ni kazi yao kwa hakika kuweza kusaidia kulinda. Kwa hivyo, hii jamii ambayo itakuwa inalinda misitu hii ambayo inasimamiwa na kaunti itasaidia pakubwa kuondoa utepetevu huo. Wale ambao watakuwa wamechaguliwa kutokana na wenyeji katika sehemu zile watasaidia pakubwa kwa sababu wao watakuwa na uchungu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Bi. Spika wa Muda, nachukua fursa hii kuunga mkono Hoja hii ya Seneta Kasanga na pia kuwahimiza Waheshimiwa wote tuangalie jinsi tunaweza kuifanya isimamiwe na kaunti zetu kupitia kwa bajeti, ambapo itakwenda kwa bunge za kaunti kuhakikisha kwamba hii mapendekezo ya Bunge la Seneti yametekelezwa. Asante, Bi. Spika wa Muda."
}