GET /api/v0.1/hansard/entries/947749/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 947749,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/947749/?format=api",
    "text_counter": 125,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "ya kubeba makasha, wafanyibiashara wetu hivi sasa hawawezi kufanya biashara kwa njia huru. Kwa maana hiyo, inakuwa hujuma ya kiuchumi. Nikiwa Mbunge wa Jomvu, ninasema hatutakubali jambo hili. Lazima Serikali iweke huru ufanyaji wa biashara. Watu watumie njia yoyote ile wanataka kutumia. Ikiwa mtu anataka kutumia malori, atumie malori. Ikiwa mtu anataka kutumia SGR, atumie, lakini kulazimishana isifanyike katika nchi hii. Serikali imesema kuwa imesimamisha mambo haya lakini tunaona mambo haya bado yanaendelea. Juzi kuna watu waliofanya maandamo na wameshikwa. Nikiwa Mbunge wa Jomvu ambapo wafanyibiashara wa malori wengi wapo, ninasema leo sisi watu wa Mombasa tutaichukulia hatua Serikali ya Kenya ikiwa haitaki kutusikiza. Tutapeleka mashtaka katika Korti ya Afrika Mashariki. Afrika Mashariki ina haki ya kusikiza shida yetu ikiwa nchi yetu haiwezi kutusikiza. Kando na Afrika Mashariki hata International Criminal Court (ICC), tunaweza kuenda kwa sababu hii ni hujuma. Hatuwezi kuishi katika hujuma ya kiuchumi. Watu hawana kazi. Watu hawawezi kusomesha watoto sasa. Hivi sasa, watu hawawezi kuishi katika nyumba zao. Kwa hivyo, ninachukua fursa hii kusema ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu utawezesha kuona kuwa mambo ya economic crimes yamechukuliwa kwa hali ya sawasawa. Ahsanteni sana."
}