GET /api/v0.1/hansard/entries/948274/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 948274,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/948274/?format=api",
    "text_counter": 373,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taveta, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Kwanza, wafanyikazi wengi wanaokwenda nchi za nje wanakwenda kwa makusudi ya kupata kazi. Lakini njia wanayotumia sio mwafaka ambayo Serikali yetu ya Kenya na serikali hizo za nje zinaweza kufuatilia kuangalia na kuhakikisha kuwa watu hawa wamefika kule kwenda kufanya kazi. Kwa sababu wametoka nchini kwa njia ambayo sio halali, wakiwa kule nje, wanajificha sana. Hata wakiwa na matatizo, wanaogopa kwenda kwenye Ubalozi wetu kueleza matatizo yao. Vile vile, utakuta kuwa wanaotaka kulalamika majina yao hayako kwenye maeneo walikoorodheshwa. Hivyo basi, watu huvumilia matatizo waliyonayo. Kamati ilienda ikakuta kuwa wanaokwenda bila kutangaza wanakokwenda na bila kutafuta njia mwafaka inayofaa ya kwenda kutafuta kazi kule vile vile watasaidika."
}