GET /api/v0.1/hansard/entries/948275/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 948275,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/948275/?format=api",
    "text_counter": 374,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taveta, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Ingekua vizuri nafasi ambazo ziko kule nje ziwekwe wazi na wale mawakala ama wanaosimamia upande wa kutafuta wafanyikazi wawe watu ambao Serikali yetu inawafahamu vizuri. Inafaa wawe wamesajiliwa hapa na kule. Hivyo basi mtu akitoka hapa akiwa amepitia kwa mawakala, itakuwa rahisi upande ule mwengine kujua kuwa mtu ambaye amechukuliwa na kupatiwa nafasi amepitia wakala fulani. Jambo hili lina utatanishi na matatizo. Ukweli ni kwamba watu wanaofanya kazi kule nje, na haswa Wakenya, wameteseka. Wengine wameteswa mpaka wakapoteza maisha yao. Wanavumilia wakiteseka kwa sababu hawawezi kusema wanajua hawakuenda kwa njia zinazofaa."
}