GET /api/v0.1/hansard/entries/948276/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 948276,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/948276/?format=api",
"text_counter": 375,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Mara nyingi upande wangu wa Taveta, nimewakanya vijana wengi wanaotaka kuenda kufanya kazi nje kwa njia zisizo sawa. Mara nyingi wakifika kule wakianza kupata shida, tena wananipigia simu wakiniambia niliyowakanya yanatokea. Hivyo basi, inakuwa shida sana kumsaidia mtu akiwa mbali. Waswahili wanasema fimbo ya mbali haiui nyoka. Hivyo basi inakua shida kwetu sisi kuwasaidia wakiwa katika nchi za kigeni. Lakini kiserikali na kisheria, na haswa Wizara inayosimamia masuala ya Wafanyikazi na Wizara ya Nchi za Kigeni, wanyooshe barabara ili wanaosafiri kwenda nje waende kwa njia inayofaa na mwafaka. Mawakala wanoshgulikia masuala haya wawe wamesajaliwa ndio iwe rahisi watu kujua mahali kila mtu amewekwa kwenye kazi ili iwe rahisi kufuatilia."
}