GET /api/v0.1/hansard/entries/948293/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 948293,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/948293/?format=api",
    "text_counter": 392,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Wale wanaoenda kufanya kazi kule wanafaa watengeneze jina la Kenya. Kuna wengi wanaotaka hizo nafasi, wamekaa mitaani na hawajazipata. Wakitengeneza jina la Kenya, wataiuza Kenya na wengine watapata nafasi ya kuenda kule. Kuna matatizo lakini pia kuna watu walio na matatizo. Kwa mfano, kama umeenda kufanya kazi, nenda na ile kazi yako ilivyoandikwa kwenye mkataba lakini ukienda kule na kufanya kazi tofauti, wewe umetumia tu njia ya kufika kule kisha ufanye kazi zako. Kwa mfano, kuna wengine wameenda nchi za Arabuni kisha unasikia wanauza pombe na serikali ya kule hairuhusu. Hata kama hairuhusiwi, itakuwa hatia. Utajitafutia shida mwenyewe kisha uanze kupiga simu usaidiwe. Yametokea mengi hata hapa Kenya. Unachukua msichana wa kazi na badala ya kufanya kazi ya nyumbani, anakuja kazi ya kutafuta bwanako. Utakubali? Hayo matatizo yanatokea huko pia. Yakitokea, lazima kutakuwa na matatizo. Shida ziko na mimi ningeomba ubalozi wa Kenya kule uwasaidie. Pia kuna wengine wanapata matatizo ambapo pengine kosa la mtu mwingine linawashukia. Katika hali kama hizo, tunaomba ubalozi wetu ushirikiane zaidi na uangalie kwamba wale watu walio kule wasipate matatizo. Kuna wengine wanapata matatizo mpaka ukiuliza pengine kazini hayupo na Kenya haitaki kumrejesha. Shida kama hizo pia ziko."
}