GET /api/v0.1/hansard/entries/948294/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 948294,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/948294/?format=api",
"text_counter": 393,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "Pia nimeona Kamati ikisema kwamba inataka sasa kazi zipitie kwa Wizara ya Leba ili isije ikaleta shida ikawa kaunti zingine hazipati nafasi. Saa hii kama sisi watu wa Lamu, mila za kule wengine zawashinda lakini sisi hazitushindi. Saa hii tunapata hizo nafasi za kuenda kule. Zikija kwa Wizara, isije wakapea wengine na sisi tukazikosa. Wale ambao hawawezi mila za kule wasiende. Wale wanaoweza waende. Kwa sababu ni mila za Kiislamu, wengine zinawashinda. Kwa mfano, wanataka wavae hijab ama mtandio, wakifika kule lakini wengine wanataka kuvaa nguo zao. Kama zile ndizo zinaleta shida, afadhali wasiende na watafute nchi zingine ambazo mila ni kama zile. Hilo la kuleta kwa Wizara ya Leba, siliungi mkono maanake wengine watakosa hizo nafasi. Asante."
}