GET /api/v0.1/hansard/entries/948794/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 948794,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/948794/?format=api",
    "text_counter": 376,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niunge mkono Hoja iliyoletwa na Sen. Kasanga. Nampongeza Sen. Kasanga kwa kuleta Hoja hii, ambayo madhumuni yake ni kuwa na makundi ya kijamii ya kukuza miti, ambayo ina faida nyingi katika nchi yetu na ulimwengu nzima. Tunafahamu kwamba dunia bila miti sio dunia. Dunia ikikosa miti, itakuwa jangwa na hakutakuwa na maisha mazuri. Tuna jukumu la kuweka sheria ambayo itakuza miti katika kaunti zote 47. Tunapaswa kuweka asilimia fulani ya fedha za kaunti kwa sababu ya kukuza makundi ya jamii ambayo yanakuza miti. Madawa yote duniani yanatokana na miti. Madawa ya mitishamba yanavuma zaidi ulimwengu mzima. Maisha ya wanadamu inategemea miti."
}