GET /api/v0.1/hansard/entries/948796/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 948796,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/948796/?format=api",
"text_counter": 378,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, miti huvunja upepo mkali, ambao ni hatari katika maisha ya mwanadamu kwani inaharibu mali. Penye miti mingi hata kuwe na upepo mkali unaoweza sababisha uharibifu wa mali, miti husaidia pakubwa. Na katika hali hiyo ambapo sisi, kama Seneti, tunafaa kuweka sheria kama hii iliyoletwa na Sen. Kasanga siku ya leo. Tuna haki ya kuunga mkono Hoja hii hili nchi ya Kenya iwe na miti. Kwa hakika, palipo na miti pana maisha mazuri. Dunia bila miti inakosa urembo na hewa safi. Kwa hivyo, tukipanda miti mahali penye janga, ukali wa jua utakosekana na pahali hapo patakuwa pasafi pa wanadamu kuishi."
}