GET /api/v0.1/hansard/entries/949193/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 949193,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949193/?format=api",
    "text_counter": 388,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninataka nianze kwa kuwapongeza wanakamati kwa kazi waliofanya, lakini ninataka kusimama kwa msimamo wa kupinga Ripoti hii. Waswahili husema “mficha uchi hazai”. Ndugu zetu wamepewa kazi hii, sababu kubwa ni mateso ambayo Wakenya wamekuwa wakipitia katika nchi hiyo. Nikiwauliza Waheshimiwa, ni kwa nini hawakupelekwa nchi nyingine ilhali kuna Wakenya wanaofanya kazi katika nchi nyingine pia? Kwa nini wakapelekwa Saudi Arabia kuchunguza mambo fulani, hususan yale yanayojiri; Wakenya wanavyokufa kwa njia zisizoeleweka? Ni masikitiko makubwa sana kuona kwamba nchi yetu yaendeshwa bila utaratibu. Leo hii tunaambiwa kuna Wakenya wanaenda kule kwa njia ambazo hazieleweki. Lakini Mkenya yule yule ambaye anarudishwa akiwa mzigo baada ya kuuliwa na mwajiri wake kule Saudi Arabia, utapata ako na mkataba na visa inayoonyesha kwamba alienda kule kufanya kazi. Kamati imetueleza kwamba ilipata idadi ya Wakenya wanaofanya kazi kule ni takriban 55,000. Lakini ninataka kusema kwamba idadi hii, wakija katika stakabadhi za rekodi ya Wizara ya Wafanyikazi hapa Kenya, watakuwa hawajui na hawajielewi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}