GET /api/v0.1/hansard/entries/949248/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 949248,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949248/?format=api",
    "text_counter": 41,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Mheshimiwa Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa sheria ya wauzaji bidhaa reja reja barabarani. Mswada huu umekuja wakati muafaka kabisa kwa sababu tumeona kwa muda mrefu wachuuzi wengi ambao wanafanya biashara zao ndogo ndogo barabarani wanasumbuliwa na maafisa wa kaunti pamoja na polisi kwa sababu hawana sehemu maalum waliyotengewa kuweza kufanya biashara zao. Inatakikana ikumbukwe kwamba katika biashara hizi, kila mfanyabiashara ameekeza rasilmali yake. Rasilmali ile inamsaidia kupata chakula cha kila siku na kusomesha watoto wake na wale wanaokaa katika miji ambao wamepangisha nyumba, inawasaidia pia kuweza kulipa kodi za nyumba na kuishi maisha yanayofaa kwa binadamu. Pia itakumbukwa kwamba hii ni biashara moja kubwa sana kwa sababu katika kila kaunti na kila mji, kuna wafanyabiashara kama hawa ambao wanafanya biashara kila siku kuweza kuendesha maisha. Kwa hivyo, inachangia pakubwa uchumi wa nchi yetu ya Kenya. Ijapokuwa inasemekana kuwa biashara haina mwongozo, lakini tunahitaji kutunga sheria ambayo itawapa mwongozo wafanyabiashara kama hao. Bw. Spika, watu wengi wamedharau biashara hii kwa misingi kwamba inafanywa na watu wadogo wadogo ambao mara nyingi hawana kazi nyingine ya kuwapatia chakula. Lakini kwa kazi wanayofanya, ni kazi kubwa kwa sababu inasaidia pakubwa kupunguza ukosefu wa kazi, kuleta bidhaa karibu na wananchi. Kwa sababu mara nyingi, bidhaa nyingi zinakuwa shida kupatikana. Biashara hizi zinasaidia wale wenye biashara kubwa wanaoleta mali kwa wingi kuweza kupata njia rahisi ya kufanya biashara yao na kuregesha rasilmali zao bila kutatizika. Ni lazima sheria iweze kusaidia wafanyabishara hao ili wasinyanyaswe na kudhulumiwa na maafisa wa kaunti ambao wanajaribu kuchukua fedha na mali zao kiholela. Ipo haja katika miji yetu kubwa kwa sababu soko ambazo zimejengwa mpaka sasa hazitoshi kuwafaidi wafanyibiashara wote. Kila siku, wafanyabiashara wapya wanachipuka ambao hawawezi kupata nafasi ya kufanya biashara zao katika soko zile. Kwa hivyo, ipo haja ya kutenga maeneo maalum ambayo wafanyabiashara watakuwa na fursa kufanyia biashara zao aidha Jumamosi na Jumapili ama katikati ya wiki baada ya saa za kazi rasmi. Kwa hivyo, sheria hii itasaidia kutatua maswala kama hayo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}