GET /api/v0.1/hansard/entries/949249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949249,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949249/?format=api",
"text_counter": 42,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Vile vile, sheria hii inaleta nafasi ya serikali za kaunti kuchukua sehemu fulani ya fedha kutoka kwa wafanyabiashara kama kodi ama leseni ambazo watalipishwa. Lakini leseni hizi zisiwe na kiwango ambacho kitaweza kuumiza wafanyabiashara hao ili faida yao yote inalipia leseni. Mweshimiwa Malalah alizungumzia kwamba kule Kakamega wanalipishwa Ksh50 kila siku ambayo inakuwa Kshs1,500 kwa mwezi, na kwa mwaka Kshs18,000 ambazo ni pesa nyingi kuliko ile ambayo mfanyabishara ambaye ana duka rasmi analipa. Kwa hivyo, sheria kama hii isitumike kuendelea kuwagadamiza na kuwanyanyasa wafanyabiashara wadogo kama hao ambao wanajitafutia nafasi ya kuishi katika ulimwengu ambao una changamoto nyingi. Inafaa pia kuangalia kwamba sheria hii itatoa nafasi ya kuwa na soko maalum ambayo tunaita kwa kiingereza periodic markets . Kwa mfano, kule sehemu za pwani, ukitembea katika kila mji katika barabara ya kuenda Lunga Lunga au Kilifi, utapata kwamba kuna soko maalum ambazo wafanyabiashara wadogo wadogo wametengewa ili waweze kupata ruzuku zao bila matatizo. Naunga mkono Mswada huu na tunatarajia kwamba, utakapopitishwa tutahakisha kaunti zetu zinafaidi pakubwa wafanyabiashara wadogo wadogo. Asante, Mheshimiwa Spika."
}