GET /api/v0.1/hansard/entries/949266/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949266,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949266/?format=api",
"text_counter": 59,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "wachuuzi hapa na pale. Pia, serikali za kaunti kwa wakati huu zimeweka askari wa kuwahangaisha wachuuzi hawa. Watu hawa wanapata dhulma nyingi sana wakifukuzwa huku na kule. Vile vile bidhaa zao hupotea na kuporwa. Ni wakati muafaka kabisa kuwa na sheria ambayo itasimamia wafanya biashara hawa ambao wanachuuza mali yao ndogo ndogo. Bw. Spika, unavyojua, kaunti zinaendelea kujengwa na tunaomba watenge viwanja vya soko maalum katika sehemu za kaunti ili wachuuzi waweze kuendelea na biashara zao."
}