GET /api/v0.1/hansard/entries/949272/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949272,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949272/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Vile mnavyojua Senior counsel ambaye tunamheshimu, baba yetu, mzee Orengo, ni mtu anayeheshimika sana. Sisi wengi tumefuata nyayo zake ndio tumekuja hapa. Sikusema kwa roho mbaya, nimesema kwa vile alikuwa anaongea na watu. Na vile tunajadili kuhusu biashara za watu wa barabarani, pia naye alikuwa katika sehemu ya kupitia na si kwa ubaya. Yeye pia ametupatia fursa hiyo. Ninafikiri naweza kuendelea. Bw. Spika, kaunti zinaendelea kujengwa na ni kweli wachuuzi wanafuata biashara katika sehemu za mabasi. Lakini vile kaunti zinaendelea kujengwa na pesa za ugatuzi zinafika katika sehemu za kaunti, ni wakati wa kuweka soko maalum na pia kutenga siku ya biashara barabarani ili watu wajue leo ni siku ya barabarani na ijulikane katika sehemu tofauti tofauti ili tuweze kuinua wale ambao wanachuuza mali yao katika barabara. Watu wengi walipitia biashara hiyo ya barabarani lakini leo hii wamekuwa matajiri. Watu wanaanza na biashara ndogo ndogo ya kuchuuza mali yao barabarani na sehemu za kusimamisha mabasi na matatu. Hivi ndivyo vile utajiri huanza. Wengi walio na maduka ya jumla siku hizi na wanaofanya katika viwanda vikubwa, wamepitia biashara ndogo za barabarani. Hivyo ndivyo walipata mali yao. Kwa sababu hiyo, ni wakati hasa wa kuwapa heshima kubwa wachuuzi wa barabarani. Bw. Spika, makali ya askari wanaowafukuza wachuuzi hapa na pale pia yavunjwe, ili wachuuzi hawa wapate pesa. Vile tunavyojua, wako na watoto katika shule za sekondari, vyuo vikuu na pia shule za msingi. Ni biashara hiyo ya uchuuzi ambayo inawawezesha kulipa karo ya watoto. Iwapo biashara ya uchuuzi itaandikishwa na ipate sheria muafaka itakayolinda biashara hiyo, basi tutakuwa tunajenga wachuuzi maskini. Hivyo ndivyo tutaweza kujenga Kenya na kuwezesha wananchi kupata mapato. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}