GET /api/v0.1/hansard/entries/949289/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949289,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949289/?format=api",
"text_counter": 82,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Sakaja",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13131,
"legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
"slug": "johnson-arthur-sakaja"
},
"content": "Bw. Spika, ni kweli kwamba wachuuzi wetu wa biashara za reja reja ni wengi sana katika miji mikuu au miji mbali mbali kama Nairobi, Kisumu, Mombasa, Nakuru na kwengineko. Hata hivyo, hawa wachuuzi wamedharauliwa kwa muda mrefu. Pia ni kweli kwamba serikali za kaunti na pia Serikali Kuu hapo awali kabla tuwe na mfumo wa ugatuzi, badala ya kusaidia wafanyibiashara kustawisha biashara zao, imekuwa ikiwadhulumu na kuwafinyilia chini. Hilo ni jambo ambalo halifai. Bw. Spika, ukitembea kila mahali katika Mji wa Nairobi, utapata vijana wetu na kina mama wakijaribu kutafuta riziki yao; wakitafuta njia ya kupeleka chakula nyumbani. Lakini kila siku ni kufukuzwa na kufungwa, ambalo ni jambo la kusikitisha. Ni kama kumekuwa na vita dhidi ya watu wadogo ama wananchi wa kawaida. Kijana, msichana mdogo ama mama wa Nairobi akiamua ajaribu kufungua biashara, anaambiwa, “Hapa panafaa kuwa na barabara;” kwa hivyo biashara yake inabomolewa. Kijana akijaribu kufanya biashara ya boda boda, anaambiwa: Ukiingia katika jiji kuu ama CentralBusiness District, boda boda yako inachukuliwa.” Bw. Spika, ukitembea hatua chache uende hapa tu katika Central Police Station, utaona idadi kubwa sana ya bidhaa za wachuuzi na bodaboda ambazo zimepigwa marufuku. Halafu tunauliza kwa nini hali ya usalama imeenda chini; tunauliza kwa nini watu wanaibiwa na wanapigwa ngeta – nafikiri tunaweza ongeza neno hilo katika Kiswahili kwa sasa – lakini bado ni Serikali hiyo hiyo ambayo inafanya watu hao wakose ajira. Wale ambao wanafanya kazi kwa matatu, wanasumbuliwa kila siku na polisi na watu wa askari wa Kaunti. Kwa hivyo, lazima tuseme kama Seneti ya kwamba hatutakubali wakenya wa kawaida waendelee kudhulumiwa. Bw. Spika, ukiangalia hata ile hela ambayo hawa wachuuzi wadogo wanatoa katika Kaunti, kwa mfano akina mama walioko Gikomba na Marikiti, kila siku wanalipa shilingi hamsini. Nilifurahi sana jana wakati Seneta wa Kakamega pia aliweza kutoa orodha kama hiyo kuhusu mji wa Kakamega. Malipo ya Kshs50 kila siku kwa siku sita, wiki nne kwa mwezi, na miezi kumi na miwili kwa mwaka ni Shilingi 14,400. Pesa hizi zote zinatozwa mfanyi biashara wa kawaida, lakini yule ambaye ako na duka analipa Ksh5,000 kwa mwaka mmoja. Kweli hiyo ni haki? Je, huu ni utu? Halafu huyo anayelipa Shilingi 14,000 bado anadhulumiwa, anafukuzwa na kupigwa. Juzi tulimuona mama mmoja ambaye ni mlemavu akiwekwa juu ya gari ya askari wa jiji eti kwa sababu ya kuchuuza bidhaa zake."
}