GET /api/v0.1/hansard/entries/949300/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 949300,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949300/?format=api",
    "text_counter": 93,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sakaja",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13131,
        "legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
        "slug": "johnson-arthur-sakaja"
    },
    "content": "Bw. Spika, shida ambayo tuko nayo ni ukosefu wa mpangilio thabiti kwa sababu kuna wale wachuuzi rejareja na pia wale ambao wana duka. Ukiangalia hao ambao tunaita hawkers ama wachuuzi wa bidhaa rejareja, sana sana wanapatikana karibu na stesheni za matatu ama pahali pa uchukuzi. Hii ni kwa sababu watu wengi wakitoka kazini jioni, wakitembea kwenda kupanda matatu, wakiona nyanya mbili hapa na vituguu wananunua. Ama mtu ataona sketi au viatu vya pumps amnunulie mke wake. Ni lazima wawe hapo karibu na sehemu za usafiri."
}