GET /api/v0.1/hansard/entries/949303/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949303,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949303/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Sakaja",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13131,
"legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
"slug": "johnson-arthur-sakaja"
},
"content": "Bw. Spika, jana nilikuwa upande wa Waiyaki Way nikaenda kula kwa kibanda pale karibu na Njuguna’s, kando ya barabara. Hao wachuuzi waliniambia ya kwamba wanadhulumiwa na kila siku wanafukuzwa. Wako mahali ambapo ni kiwanja ambacho kiko bure, hakitumiki kwa kazi yoyote. Hakuna nyumba inajengwa hapo au barabara inayopita hapo. Kuna wafanyi biashara watano au sita hivi ambao wameajiri zaidi ya akina mama na vijana 90. Lakini hivi karibuni utasikia wamefukuzwa kwa sababu ni wachuuzi wa bidhaa rejareja na hapo pahali patakaa tu wazi bila kuleta faida kwa uchumi. Hao akina mama na vijana wataenda wapi?"
}